Taarifa ya Umaskini
Halmashauri ya North Lanarkshire na NHS Lanarkhire pamoja na washirika wake katika sekta ya tatu wamejikita katika kukabiliana na umaskini na ukosefu wa usalama na kupunguza athari hizo kwa jamii zetu ili kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa fursa kwa wakazi wetu wote.
Umaskini wa kutomudu nishati
Tunajua kuwa umaskini wa kutomudu nishati ni changamoto kwa watu wengi na kwa vile wakati wa baridi unakaribia ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kupunguza gharama za nishati. Ikiwa una wasiwasi juu ya gharama zako za nishati basi msaada unapatikana. Unaweza kupiga simu Home Energy Scotland bila malipo kwa nambari 0808 808 2282 au kutuma barua pepe kwa adviceteam@sc.homeenergyscotland.org
Timu yetu ya maswala ya fedha kwa wote inaweza pia kutoa msaada na ushauri kwa vitendo kwa kaya zinazokabiliana na umaskini wa nishati.
Mikopo kwa wote
Kupunguzwa kwa pauni 20 toka kwenye Universal Credit kunaweza kuathiri uwezo wako wa kufanya malipo ya kila wakati na madeni. Ikiwa utapenda mafao yako yatazamwe vizuri au usaidiwe kuhusiana na madeni na bajeti piga simu 01698 332551 au barua pepe FIT@northlan.gov.uk au CAB yako ya karibu
Ajira
Kitengo cha kazi cha North Lanarkshire kinaweza kukusaidia kupata kazi, kuongeza masaa yako ya kazi au kukusaidia ikiwa unakabiliwa na kupunguzwa kazi au umeisha punguzwa kazi. Huduma yetu ya kusaidia wanaotafuta ajira pia hutoa msaada halisi kupitia wataalam wetu wa kazi wenye uzoefu kwa watu wenye ulemavu na wale wanaokabiliwa na changamoto za vizuizi vya kupata kazi sahihi. Msaada wetu wa kukufanya uajirike unaweza kukupatia mafunzo unayohitaji, kusaidia utunzaji wa watoto na tutakuwa pamoja nawe hata baada ya kuanza kazi. Jisajili hapa Sign-Up - North Lanarkshire's Working (northlanarkshiresworking.co.uk) au tupigie simu 0800 0730 226.
Ushauri wa Maswala ya Uhamiaji
Ikiwa wewe ni mkazi wa North Lanarkhire na unahitaji habari au ushauri kuhusu hali yako ya uhamiaji unaweza kupata ushauri wa bure wa kisheria kutoka Kituo cha Sheria cha Ethnic Minority Law Centre - piga simu 0141 204 2888
Mwisho wa Kulipwa Mshahara bila Kufanya Kazi
Kipindi cha kulipwa bila kufanya kazi kilimalizika tarehe 30 Septemba. Ikiwa hali yako ya ajira imebadilika kwa mfano, sasa hauna ajira, umepunguza masaa au umeongeza masaa na unahitaji ushauri wa kifedha / ajira au usaidizi piga simu 01698 332551 au barua pepe FIT@northlan.gov.uk au ofisi ya Citizens Advice Bureau ya mahali unapoishi.
Uanachama wa Burudani wa Active 65
Tumeanzisha uanachama wa Kuchangamsha kwa wale wenye umri wa zaidi ya miaka 65. Mpango huo hukuwezesha kutumia huduma zote bila kikomo kwenye vituo vyetu vya burudani pamoja na mazoezi, madarasa ya mazoezi ya mwili, kuogelea, vyumba vya kuboresha afya na vyote hivyo kwa Pauni 50 tu kwa mwaka mzima. Ili kujiandikisha tembelea tovuti yetu https://www.nlleisure.co.uk/new-2020/active-65 au piga simu kwa timu yetu ya uanachama nambari 01236 341969. Na kwa vijana wenye umri kati ya miaka 11 na 15 - sasa unaweza kupata uanachama wa bure wa kufanya mazoezi kwa vijana wadogo kwa miezi sita https://www.nlleisure.co.uk/active-teens